Simba SC Wameshusha Kiungo Mpya Kutoka Zambia

Simba SC Wameshusha Kiungo Mpya Kutoka Zambia
Mabingwa wa Ligi Kuu Bara nchini, Simba SC, wameshusha kiungo mshambuliaji mpya kutoka Dyanamos FC ya Zambia, Chama Clatous na taarifa zinaeleza tayari ameshamalizana na mabosi wa klabu hiyo.

Ujio wa Clatous Simba umetokana na pendekezo la Kocha Msaidizi, Masoud Djuma ambaye aliomba asajiliwa kiungo mwingine ili kuja kukupa nguvu kikosi cha Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema tayari Clatous ameshamwaga winno na atakuwa sehemu ya wachezaji wataokwea pipa kesho kuelekea Uturuki kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Simba imekuwa ikitumia jeuri ya fedha za tajiri Mohammed Dewji ambaye ndiye mwekezaji mkuu wa klabu hiyo sasa kusajili wachezaji ambapo imeamua kukipa upana mkubwa kwa ajili ya ligi na mashindano ya kimataifa.

Ujio wa Mzambia huyo unazidi kuongeza idadi ya viungo Simba ambapo baadhi wanaocheza katika nafasi hiyo ni pamoja na Shiza Kichuya, Jonas Mkude, James Kotei na  Mzamiru Yassin

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad