Simba Yafunguka Juu ya Niyonzima Kuchelewa Kambini

Simba Yafunguka Juu ya Niyonzima Kuchelewa Kambini
Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah (Try Again), amefunguka kuhusiana na kuchelewa kuripoti kwa kiungo wao, Mrwanda, Haruna Niyonzima katika klabu hiyo baada ya likizo kumalizika.

Abdallah amesema kuwa mpaka sasa wao kama viongozi hawaelewi kipi kimesababisha mchezaji huyo kushindwa kuwasili nchini ambapo alipaswa kurejea mapema ili aweze kusafiri kuelekea Uturuki.

"Likizo ya Haruna Niyonzima ilimalizika tangu July 20, lakini mpaka sasa kama uongozi hatuelewi tatizo gani limemtokea mpaka kupeleka kuchelewa kuwasili nchini hadi leo”, amesema Abdallah.

Ameongeza kuwa "Tutampa nafasi ya kumsikiliza kwasababu hatuwezi kutoa hukumu kabla ya kujua tatizo lake ni lipi, na kuhusu kwenda Uturuki kwa sasa haitowezekana kwasababu tayari yupo nje ya muda".

Niyonzima alipaswa kurejea nchini ili aweze kusafiri na wachezaji ambao ni Said Ndemla, Meddie Kagere, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga ambao walichelewa kutokana na viza zao kutokamilika mapema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad