Simba yapewa siku 75 ifanye uchaguzi Mkuu

Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ameitaka klabu ya simba kufanya uchaguzi wao ndani ya siku 75.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirikisho hilo, alisema kwamba kamati ya Uchaguzi ya TFF, wamemfikishia taarifa kwamba Simba wanatakiwa kufanya uchaguzi wao mkuu.

"Kawaida huwa ni 60 na ndivyo ninavyojua mimi, lakini Kamati ya Uchaguzi imewapa siku 75 nazani siku 15 ni za maandalizi, wanatakiwa wafanye uchaguzi wao mzima ili kupata viongozi wao," alisema.

Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba wapo nchini Uturuki wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Simba imefikia katika hoteli ya The Green Park Kartepe Resort and Spa iliyopo katika jiji wa Istanbul Uturuki na watakuwa hapo kwa muda wa siku 16 na watarudi nchini Agosti 5 siku tatu kabla ya siku ya Simba (Simba Day).

Kocha msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma alisema hali ya hewa, viwanja na mahala walipofikia ni sehemu sahihi ya kufanya maandalizi ambayo wataitumia vizuri kama walivyopanga.

Djuma alisema mazingira ya hoteli waliyofikia ni nzuri, viwanja vinakizi kufanya mazoezi magumu na mepesi au programu yoyote ambayo benchi la ufundi tutakuwa tunahitaji kufanya kulingana na mahitaji yetu ya siku.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad