“Sio Kila Tafiti ya Kupigiwa Makofi”-Lema Afunguka
0
July 10, 2018
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema amefunguka kuwa sio kila tafiti zinatakiwa kupokelewa kwa furaha bila kutafakari faida na hasara zake huku akiutilia mashaka utafiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na utafiti nchini Tanzania ya TWAWEZA.
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema.
Akizungumza na www.eatv.tv Lema amesema kuwa utafiti wa Twaweza anautilia mashaka kwakuwa umeonekana kutoa faraja upande mmoja na kuongeza kuwa huenda taasisi hiyo imefanya hivyo kwa maslahi binafsi.
“Utafiti wa TWAWEZA unapaswa kutiliwa mashaka hata kama unatoa faraja kwa kiasi fulani dhidi ya washindani wetu kisiasa,ninafikiri TWAWEZA wanatafuta zaidi uhalali kwa ajili ya siku za usoni kwa manufaa ya taasisi yao na Serikali”, amesema Lema.
Kulingana na ripoti ya TWAWEZA inadai kuwa uhuru wa kutoa maoni kwa wananchi umepungua tofauti na miaka mitatu iliyopita, huku msaada wa demokrasia ya wingi unaendelea kuwa na nguvu ambapo zaidi ya asilimia 84% wanapendekeza mfumo wa vyama vingi vya siasa.
EATV
Tags