Kutokana na matukio hayo ya kusemwa vibaya mfululizo, Steve kupitia mtandao wa Instagram ameonekana kushindwa kuvumilia na kuamua kuandika ujumbe mzito kwa wabaya wake.
Kupitia mtandao huo Steve ameandika:
Watu wengi tunamarafiki lakini hakuna kazi ngumu kama urafiki, Rafiki wa kweli ana kazi zifuatazo atasimama na wewe kwenye baya na zuri,atakuwa tayari kunyooshewa kidole kwa ajili yako, atakutetea popote pale bila kujali madhaifu yako,kwenye magonjwa njaaa hata mitihani ya kidunia atasimama nawe,Pale unapokosea rafiki anatakiwa awe mstali wa mbele kukueleza ukweli, Apende mafanikio yako,Na asiache kukumbusha mambo muhimu ya maisha. Marafiki wengi wapo kwa watu kwa sababu ya kitu fulani, wapunguze ubaki na imani ya moyo.