Sweden Yatinga Robo Fainali Kombe La Dunia

Timu ya taifa ya Sweden imeibuka na ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora Kombe la Dunia dhidi ya Switzerland iliyomalizika jana  usiku  huko Saint Petersburg huko Urusi.

Ushindi huo wa Sweden umeichukua historia ya Kombe la Dunia na kuirudisha nyuma hadi mwaka 1958, ambapo Sweden walikuwa wenyeji na walishinda mechi mbili mfululizo kwa mara ya kwanza robo fainali na nusu fainali na kutinga fainali.

Kabla ya kushinda dhidi ya Switzerland jana, Sweden ilitoka kushinda 3-0 mechi ya mwisho hatua ya makundi kwenye kundi F dhidi ya Mexico, hivyo mechi ya jana imekuwa ya pili mfululizo kwa Sweden kushinda.

Bao la Sweden limefungwa na kiungo Emil Forsberg  ambaye jana ripoti zilieleza kuwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho, alitarajiwa kuwepo uwanjani kwaajili ya kumfuatilia nyota huyo ambaye ameibuka kiungo bora wa Sweden katika miaka ya 2014, 2016 na 2017.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad