Tume ya Madini inayoongozwa na Mwenyekiti Profesa Idris Kikula imesema imebaini kuendelea kwa vitendo vya utoroshaji wa madini ya Tanzanite katika mgodi wa Mererani licha ya kukamilika kwa ujenzi wa ukuta mkubwa ulioligharimu taifa kiasi kikubwa cha fedha .
Akitoa taarifa ya ziara ya Tume hiyo katika migodi ya madini iliyopo mikoa ya Manyara, aliyeambatana na Kamishna wa Tume Profesa Abdulkarim Mruma na Mwanasheria wa Tume , anasema utoroshaji huo wa madini unachangiwa na mfumo duni wa ulinzi katika lango kuu.
Ni kutokana na upotevu huo wa madini ambao Profesa Kikula anasema umesababisha kushuka kwa mrahaba uliokuwa ukipokelewa na serikali ambao ulikuwa umepanda kwa kasi mara baada tu ya ukuta kukamilika ,tume ikatoa maelekezo yake.
Tume hiyo imesisitiza pia umuhimu wa wawekezaji kutii na kufuata kanuni na maelekezo yote ya leseni wanazopewa likiwemo suala la mahusiano na uongozi wa serikali kuanzia ngazi za vijiji na jamii inayoishi jirani ikishauri kuigwa kwa mfano wa mwekezaji wa mgodi wa madini ya Rubi wa Mundarara uliopo wilayani Longido.