Tarime kwa waka moto Mbowe, Polepole waunguruma

NA TIMOTHY ITEMBE TARIME.

KATIBU wa Itikadi na uenezi Chama cha mapinduzi (CCM),Humphrey Polepole ameweka wazi chanzo cha wanasiasa wa vyama vya upinzani kuhama vyama vyao na kujiunga na Chama cha mapinduzi kuwa ni kumkubali Rais Awamu ya Tano,John Pombe Magufuli katika kuwatetea wananchi waliowanyonge na kupiga vita rushwa.

"Wapinzani wanamkubali Rais awamu ya Tano,John Pombe Magufuli kwa mpango wake kupambana na rushwa na kuwakumbuka wanyonge lakini kitendo cha baadhi ya wapinzani wachache kurusha maneno kuwa wanao hama vyama vyao na kuhamia CCM wamenunuliwa nikitendo ambacho hakina ukweli ndani yakealisema"Polepole.

Kauli hiyo aliitoa jana katika uzinduzi wa kampeni wakati akimnadi mgombea udiwani kata ya Turwa Chacha Mwita Ghati wa Chama cha mapinduzi baada ya aliyekuwepo,Zakayo Chaha Wangwe  kupitia Chama cha Demokorasia na maendeleo Chadema kujiuzulu na kuhamia CCM kwenye mkutano ambao ulifanyikia viwanja vya Rebu Senta huku Chadema ikizingulia viwanja vya Rebu sokoni.

Polepole aliongeza kuwa wananchi waliona macho wanatazama maendeleo yanayofanyika ndani ya utawala wa awamu ya Tano inayoongozwa na John Pombe Magufuli jambo ambalo linawafurahisha baadhi ya wapinzani kuachia ngazi na nyadhifa walizonazo na kuhamia CCM.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoani Mara,Samweli Keboye maarufu namba tatu alisema kuwa utendaji kazi mzuri wa Rais Magufuli umekibeba Chama cha mapinduzi na hawanashaka katika uchaguzi wa maruio ndani ya kata ya Turwa wananhi wankiamini chama na watawapa kura.

Wakati huo huo,Mwenyekiti Chadema Taifa Freeman Mbowe  alitupia lawana Chama cha mapinduzi kuwa kinawanunua wapinzani sababu inayofanya wahamie CCM.

"Mimi tu nimewashinda wanachama cha mapinduzi kutofika Bei kwahalli hiyo wanapanga usiku na mchana ili kuhakikisha wananinunua jambo ambalo kwangu halitatokea wananchi mnatakiwa kuwa makini na wanaccm"alisema Mbowe.

Pia Mbowe alionyesha mashangao wake kwa serikali ya awamu ya tano kununua ndege ya mabilioni huku wananchi wake wanaukata wa maisha jambo ambalo alisema kununua ndege ya shilingi Bilion 680 hali wananchi wa Tanzania wanakula mlo mmoja kwa siku ni kitendo ambacho hakikubaliki.

Mbowe aliwataka wanaTurwa kutomwangusha na kumpigia kura zote za ndio mgombea udiwani kata ya Turwa wa Chama chake cha Chadema,Charles Mnanka.

Naye Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini,Esther Matiko aliwataka wananchi kumuunga mkono na kuendelea kumwamini ili kupiga kurwa kwa Chadema ili waendelee kuongoza halmashauri ya Mji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad