TCRA yafichua sababu zinazopelekea kufungia wasanii


Ikiwa imepita siku moja tangu Mamlaka ya Mawasiliano TCRA) kuwapatia adhabu wasanii  Irene Uwoya na mwenzake wa mitindo, Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema sababu ya Mamlaka kuwa inatoa adhabu ni kutokana na Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo kuwa na hadhi ya kimahakama kisheria. 

Mwakyanjala amesema wakati ilipotaka kufahamu ni hatua gani zaidi ambazo Mamlaka hiyo itakuwa inachukua dhidi ya wasanii ambao watakuwa wanakiuka sheria hiyo ya mitandao na kanuni za maadili ya mwaka 2018 licha ya wasanii wengi kuonywa. 

Amesema kwamba licha ya kwamba wasanii wamekuwa wakipigwa faini, maonyo makali lakini pia maamuzi yanayotolewa huzingatia sheria za kimahakama kwa kuwa Kamati inamamlaka na ndiyo maana hutoa nafasi ya rufaa. 

"Ninachoweza kusema kwa sasa, wasanii wanaadhibiwa na sheria na pia wanapewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 21, baada ya hapo kama atakuwa ameridhika ndipo mambo mengine yanaweza kuongelewa. Hata jana waandishi hatukuweza kuwaruhusu kuuliza maswali kwa kuwa jambo hili bado lipo chini ya sheria, baada ya siku 21 kuisha vyote ulivyokuwa unataka kujua utafamu kwa kuwa itakuwa imeshajulikana kama wamekubaliana na adhabu au laa."  Mwakyanjala. 

Mnamo Juni 20, 2018, Msanii Irene Uwoya alichapisha picha kwenye mtandao wake wa kijamii ikiwa inamuonyesha maungo yake ya ndani huku yeye mwenyewe akidai alikuwa ufukweni ndio maana alifanya hivyo. 

Kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano (TCRA) hivi karibuni imekuwa ikiwachukulia hatua wasanii wanaokiuka sheria za mitandao iliyotungwa 2010, ambapo kanuni zake zilianza kutumika 2018.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad