Tetemeko laua watu 14, watalii wasimulia


Watu 14 wamepoteza maisha baada ya tetemeko kupiga eneo maarufu la utalii nchini Indonesia 

Tetemeko la ukubwa wa 6.4 lilitokea kisiwa la Lombok siku ya Jumapili 

Kisiwa hicho huwavutia watalii kutoka duniani kote kutokana na fukwe zake za kuvutia na maeneo ya kutembea, eneo hilo liko umbali wa kilometa 40 mashariki mwa Bali. 

Zaidi ya watu 160 wamejeruhiwa na maelfu ya makazi yameharibiwa, maafisa wameeleza. 

Mtalii raia wa Malaysia aliyekua akitembea kuelekea mlima Rinjani ni miongoni mwa waliopoteza maisha. 

Utafiti wa wataalamu wa Jiolojia nchini Marekani ulisema tetemeko lilipiga umbali wa kilometa 50 Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Mataram. 

Kisha likafuatiwa na matetemeko madogo zaidi ya 60, kubwa likirekodiwa kuwa na ukubwa wa 5.7. 

Sutopo Purwo Nugroho, Msemaji wa taasisi ya kukabiliana na majanga, amesema kuwa madhara mengi hujitokeza pale watu wanapoangukiwa na vifuri au mawe 

''Sasa tunachokitazama na kuwaokoa watu.Baadhi ya waliojeruhiwa bado wanapata matibabu kwenye vituo vya afya'', alieleza 

''Tetemeko lilikuwa na nguvu....watalii waliingiwa na hofu na kuanza kuondoka hotelini'',Lalu Muhammad Iqbal afisa kutoka wizara ya mambo ya nje aliiambia BBC. 

''Matetemeko yalikuwa na nguvu ''niliona mawimbi kwenye bwawa la kuogelea hotelini, tulikimbia nje ya hoteli''. 

''Dakika 30 baadae kulikuwa na tetemeko la kwanza.Watu waliingiwa na hofu kwa kuwa nyumba nyingi zimetengenezwa kwa mbao na bamboo, lakini watalii walikuwa na hofu zaidi. 

Watalii wa UK , Katherine and Alexis Bouvier, ambao walilkuwa kwenye fungate wameiambia BBC: ''tuliamshwa na tetemeko la ardhi majira ya saa sita usiku, ilikua inaogopesha''. 

maporomoko ya ardhi yamekata mfumo wa usambazaji maji na umeme katika baadhi ya nyumba, walieleza. 

''Tumepishana na magari kadhaa ya maji tulipokuwa tukielekea kusuni.Walituambia kuwa udongo wa saruji ulikuwa unadondoka kutoka sehemu ya dari na nyufa zikaanza kujitokeza kwenye majengo''. 

Hifadhi ya mlima Rinjani,imefungwa kutokana na maporomoko ya ardhi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad