TETESI: Mkwasa ajiuzulu nafasi ya Ukatibu Mkuu Yanga, jitihada zafanyika kuwabakiza Yondani na Kessy


Inaelezwa kuwa Katibu Mkuu wa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameamua kujiuzulu nafasi yake ndani ya timu hiyo kongwe nchini.



Mkwasa ametangazwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo mnamo Februari 1 mwaka 2017 na kujaza nafasi iliyoachwa wazi kwa muda mrefu iliyokuwa ikikaimiwa na Baraka Deusdedith baada ya kuondoka kwa Dkt. Jonas Tiboroha.

Charles Boniface Mkwasa aliwahi kuwa kocha wa klabu hiyo kabla ya kuwa kocha wa Taifa Stars.

Na Klabu ya Yanga imemuita beki wake wake, Kelvin Yondani pamoja na Hassan Kessy kwaajili ya mazungumzo baada ya kuwepo na uvumi wa wachezaji hao huenda wakajiunga na mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu 2017/18.



Habari zisizo rasmi zinaeleza kuwa Yondani alishamalizana na Simba kilichobaki ni kukabidhiwa kitita cha fedha tu ili kusaini mkataba lakini uongozi wa Yanga wanapambana kufa na kupona ili kuhakikisha dili hilo halikamiliki.

Ikumbukwe kuwa wachezaji hawa wote wawili wanao husishwa na kutimkia Simba hawajasafiri kwenda nchini Kenya kuikabili Gor Mahia kwenye mchezo wa kombe la shirikisho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad