Kampuni hiyo imefikia hatua ya kufanya maamuzi hayo kutokana na walinzi wake kuzidi kufanya kazi katika ofisi ambazo haziwalipi chochote, jambo ambalo kampuni imeeleza ni kama wanateseka bure.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Sunday Marwa, amefunguka na kusema wanaidai TFF kiasi cha fedha zaidi ya milioni 50 za kitanzania ambazo zinapaswa kulipwa ili huduma ya walinzi kufanya kazi iendelee.
Marwa amesema wameamua kufanya hivyo kwa maana deni lingekuwa kubwa na hivyo imewabidi wafanye hivyo ili lisizidi kuongezeka.
Mbali na ofisi hizo, Marwa amesema Kiwango Security iliingia mikataba miwili na TFF ambapo walinzi walikuwa wanazilinda ofisi za TFF pamoja na kwenye makazi ya Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia.
Kiongozi huyo ameeleza walinzi wameondolewa sehemu zote mpaka kwa Rais Karia akisema kuwa wao ni binadamu pia na hawawezi kuendelea kufanya kazi kama mashine bila kulipwa.