TFF Yakubali Kulipa Deni la Milioni 50 Linalodaiwa na Kampuni ya Ulinzi

TFF Yakubali Kulipa Deni la Milioni 50 Linalodaiwa na Kampuni ya Ulinzi
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa litaanza kulipa taratibu deni la takribani zaidi ya shilingi za Kitanzania, milioni 50 ambalo wanadaiwa na Kampuni ya Ulinzi (Kiwango Security).

Hatua hiyo imekuja kufuatia kampuni kuondoa walinzi wake wote kwenye ofisi hizo zilizopo mitaa ya Karume, Ilala, Dar es Salaam pamoja na kwenye makazi ya Rais wake, Wallace Karia.

Kufuatia tukio hilo  Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema watajitahidi kulipa deni la kampuni hiyo kwa taratibu za kiofisi ili walinzi hao waweze kurejea tena kuendelea na kazi kama mwanzo.

“Ni  kweli tunadaiwa na hivyo itatupasa tuanze kulilipa deni hilo taratibu mpaka watakapolikamilisha ili huduma iendelee”, amesema Kidao.

Zimepita siku kadhaa ambapo Mwenyekiti wa uendeshaji katika kampuni hiyo, Sunday Marwa, aliposema wameondoa wafanyakazi wao na hawatoweza kuwarudisha mpaka pale watakapolipwa fedha zao.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad