Thailand Yasaka Njia ya Kuwaokoa Vijana 12 Waliokwama Kwenye Pango

Thailand Yasaka Njia ya Kuwaokoa Vijana 12 Waliokwama Kwenye Pango
Wavulana kumi na wawili pamoja na kocha wao mmoja waliokwama katika pango moja lililojaa maji nchini Thailand wamepokea chakula cha kwanza tangu walipokwama pamoja na dawa kitakachodumu kwa siku kumi.

Wazamiaji saba, pamoja na daktari mmoja na nesi mmoja watakaokuwa wanafuatilia hali za afya zao humo pangoni , wameungana na na kikundi kilichomo pangoni upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya kugundua kuwa timu hiyo iko hai mwanzoni mwa wiki hii.

Wazamiaji kwa sasa wanabangua bongo ni kwa namna gani iliyo bora zaidi watakavyo fanikisha kulitoa kundi hilo pangoni hadi seheme ya usalama.

Mvua nyingi zinazonyesha zinaashiria kiwango cha maji kujaa na kuhatarisha maisha ya watu waliomo pangoni pamoja na mifuko ya hewa waliyonayo mahali waliko kama mateka.

Wavulana hao waligunduliwa siku tisa baada ya kuingia pangoni humo huko katika jimbo la Chiang Rai kufuatia mafunzo ya mpira waliyokuwa wakifanya na kujikuta wakikwama pangoni kutokana na kina cha maji kuongozeka kulikosababisha na mvua nyingi zinazonyesha.

Mapema wiki hii, Maafisa wa serikali nchini Thailand waliwaambia waandishi habari kwamba wakoaji wameanza na zoezi la kuchunguza afya za kundi hilo pamoja na matibabu, na pia kuwaburudisha vijana hao na kuarifu kuwa hakuna hata mmoja mwenye afya mbaya miongoni mwa waliokwama pangoni.

Wavulana hao walipewa chakula chepesi kwa kuanzia ambacho ni rahisi kusagika tumboni, chenye kuongeza nguvu kwa haraka , chenye wingi wa vitamini na madini mwilini. Chini ya uangalizi makini wa madaktari, anaarifu Apagorn Youkonggaew ambaye ni mkuu wa vikosi maalumu vya uokozi nchini Tailand wakati wa mkutano baina yake na waandishi habari.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad