Mamlaka ya Kukusanya kodi TRA imeonya wafanyabiashara wanaotoa risiti feki za EFD kwani hawataondolewa msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi,hivyo watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.
Kamishna wa Kodi za ndani TRA Elijah Mwandumbya amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara jijini Arusha ambapo amewataka wafanyabiashara kuepuka kutoa risiti feki kwani ni kosa kisheria hivyo serikali haitawafumbia macho.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara mkoani Arusha TCCIA ,Walter Maeda wamesema kuwa wamemshukuru Raisi Maufuli kwa kuwaondolea madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu zake.
Kwa upande wake Mfanyabiashara Nicholous Duhia ameiomba serikali kupanua wigo mpana wa msamaha huo kwa wafanyabiashara wenye malimbikizo ya miaka ya nyuma ili waweze kuanza upya vizuri na kulipa kodi ili kuisaidia serikali kupata mapato yake.