Rais wa Marekani Donald Trump amesema anakubaliana na hitimisho lililotolewa na Taasisi za Ujasusi za nchi yake kwamba Urusi iliingilia kati uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wa mwaka 2016.
Akikanusha kauli yake aliyoitoa siku moja iliyopita baada ya mkutano wake na Rais Vladmir Putin wa Urusi.
Amesema alieleweka vibaya siku ya Jumatatu na kwamba alikuwa akimaanisha kwamba hakuona sababu kwanini isiwe Urusi ambayo ilifanya udukuzi katika uchaguzi huo.
Obama aonya dhidi ya viongozi wababe, azungumzia Ufaransa
Kamera zinazotambua iwapo una raha ama wewe ni tishio
Ni Rais Trump akiitolea ufafanuzi na kuikanusha kauli yake ya awali, ambayo imezua sintofahamu na kukosolewa vikali. Hata kwa baadhi ya washirika wake wakitaka ufafanuzi zaidi na kusafisha kauli hiyo.
Amedai kuwa katika mkutano huo wa Helsinki alimaanisha kusema kwamba hakuna sababu ya kufikiria kuwa Moscow haiwezi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.
Amesema ana imani na kuunga mkono taasisi za usalama za nchi yake.