Ukaguzi wa Magari Kilimanjaro wabaini Madereva kutumia Leseni za ndugu zao


UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa  wa Kilimanjaro umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya abiria ukiwemo kuendesha bila  Leseni ,Umri  wa kuendesha gari kupitiliza , wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao. 

Katika kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria yaendayo mikoani na yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu  Operesheni kikosi cha usalama Barabarani ,Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi. 

Katika ukaguzi huo magari zaidi ya 800 yamekaguliwa na yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku  baadhi ya Madereva wakikutwa  na silaha katika magari yao vikiwemo Visu,kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki. 

Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani ,Mkaguzi wa Polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la kupunguza ajali  huku baadhi ya Madereva na wananchi wakipongeza utaratibu huo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad