Uongozi wa klabu ya Yanga umesema upo kwenye harakati za kumsaka mbadala wa Shadrack Nsajigwa ambaye alikuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo.
Nsajigwa maarufu kama Fuso aliachana na Yanga kwa madai ya kuwa alikuwa anahitaji kupumzika hivyo ilifikia uamuzi wa kuamua kujiuzu nafasi hiyo kuwapa nafasi wengine.
Nsajigwa alikuwa sehemu ya benchi la ufundi Yanga tangu aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mzambia George Lwandamina ambaye aliondoka klabuni hapo kimyakimya bila kuaga.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kumapata mbadala wa Nsajigwa na pale atakapopatikana watakuwa tayari kumtangaza siku za usoni.
Wakati kikosi cha Yanga kipo kambi hivi sasa kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa Julai 18 2018 jijini Nairobi.