Ushamba chanzo cha kutoendelea Tanzania


Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa Chama cha Wananchi  CUF, Julius Mtatiro amesema, Tanzania inaonekana kuchelewa kusonga mbele kutokana na ushamba wa viongozi na kutojali vizazi vijavyo ndiyo maana mpaka sasa hoja ya uraia pacha inashindwa kupitishwa.


Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa Chama cha Wananchi  CUF, Julius Mtatiro.

Mtatiro amesema kwamba sheria zilizopitwa na wakati ndizo zinafanya sheria ya Uraia pacha kwenye Katiba kushindwa kufanyiwa marekebisho, na hata wakati wa mabadiliko ya katiba kulikuwa na ukiritimba wa ung'ang'anizi wa mambo ya kale yaliyopelekea isibadilishwe.

Mtatiro amesema kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, Tanzania ilipaswa kuwa na Uraia pacha  ili kuwaruhusu watu wanaopenda kuwa na uraia wa Tanzania wapate na hiyo ingesaidia hasa pale ambapo wangeamua kufanya uwekezaji na hata katika suala zima la ulipaji kodi.

"Hizi siyo zama za kina Nyerere na Uhuru, hizi ni zama ambazo kila nchi serikali inajitanua kutumia rasilimali za ndani na nje kupanua uchumi wa nchi yake" Mtatiro.

"Roho mbaya, ukale na ushamba pamoja na kuwa na viongozi wasiokuwa na 'focus' kwa vizazi vijavyo ndiyo maana kama Taifa tunaonekana tumechelewa" ameongeza

Hata hivyo Mtatiro anashangaa kuona kwamba suala la usalama linahofiwa katika suala la uraia pacha, wakati kama mtu mwenye uraia wa nchi akiiba au akiua ataweza kukamatwa mahali popote alipo kutokana na teknolojia kukua duniani kote hivyo hakuna haja ya serikali kuhofu.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad