Kufuatia mabadiliko mbalimbali yaliyotangazwa na BASATA kwa wasanii wa muziki na waigizaji wa filamu nchini Tanzania, Rapper Nikki Mbishi ameibuka na ushauri kwa wasanii wa muziki.
Rapper Nikki Mbishi kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa kwa sasa wasanii wa muziki watafute kazi nyingine ya kufanya kwani ya sanaa ya muziki nchini imeshakufa na hakuna namna.
“Kwanza kampuni zenyewe hazitoi deals kwa wasanii directly mpaka middleman ahusike na analipwa cha udalali bado BASATA nao wanataka hapo hapo duh, wasanii tutafute cha kufanya sanaa ishakufa, chemchemi za mapato zinazidi kukauka..Ukisoma ajira hakuna,ukijiajiri vikwazo juu ya vikwazo mpaka ujasiriamali unakushinda,mbona awamu tutarudi vijijini kuchoma mkaa na Best Nasso japo Wizara ya mali asili na utalii nayo itakuja kubana tena.“amesema Nikki Mbishi na kuifungukia serikali.
“Laiti Serikali ingetazama uwiano wa waajiriwa na waliojiajiri isingeweka terms kandamizi kiasi cha watu kujipiga mpaka risasi wenyewe maana tunakoelekea Mungu sitiri..Nchi yako mwenyewe ila unaweza hata kukufuru ukajiuliza “Hivi mimi nafanya nini hapa Duniani?”. Kuna siku biashara ya muziki wetu itakuwa kama ile ya kuuza madawa ya kulevya tu,maana utaambiwa santuri zako zote HARAM.“ameandika Nikki Mbishi.
Kwa upande mwingine Nikki wa Mbishi ameenda mbali zaidi na kudai kuwa kama kungelikuwa na uwezekano basi Mungu angepeleka miaka 20 mbele ili kuwe na uwezekano wa kuivunja BASATA kwani haipo kwa ajili ya kulea wasanii.
“Mungu angepeleka mbele miaka hata 20 leo iwe 2038 labda tungeanua matanga ya mawazo mfu tupate mawazo mapya yenye manufaa kwa kizazi kilichopo..Vunja BASATA jenga hata BAR watu walewe maana haitulei bali inatutesa tu,“ameandika Nikki Mbishi.