Vyombo vya habari vya taifa nchini Uturuki vimetangaza kwamba serikali imeondoa hali ya hatari iliyowekwa nchini humo kufuatia mapinduzi yaliyoshindwa miaka miwili iliyopita.
Katika kipindi hicho makumi kwa maelfu ya watu walikamatwa na kushikiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka chini ya agizo la Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.
Wanajeshi, Polisi, Raia, Waandishi wa Habarai na walimu ni miongoni mwa waliokamatwa.
Maelfu wengine ikiwemo majaji kadhaa waliachishwa kazi zao.
Reli mpya ya SGR nchini Kenya yasababisha hasara ya shilingi bilioni 10
Mfanyakazi azawadiwa gari na mwajiri wake baada ya kutembea umbali wa kilomita 32
Zawadi ya Magufuli kwa Obama na mambo mengine makuu
Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema kuondolewa kwa hali hiyo ya hatari pekee hakuwezi kbadili hatua kazli za kisiasa zilizochukuliwa ambazo ziliibadili nchi hiyo na kuifanya inayokandamiza haki za binadamu.
Mapema mwezi huu Rais Erdogan aliapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.