Uvumbuzi wa Chanjo ya Ukimwi waipa wanasayansi changamoto


Chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi ambayo ina uwezo wa kuwalinda watu duniani kutokna na virusi hivyo imeonyesha matumaini. 

Tiba hiyo inayolenga kutoa kinga dhidi ya virusi kadhaa, ilitoa kinga ya Ukimwi katika majaribio yaliofanyiwa watu 339, kulingana na utafiti mmoja uliochapishwa katika jarida la Lancet. 

Pia iliwalinda tumbili dhidi ya virusi vinavyofanana na vya ugonjwa huo. 

Majaribio zaidi sasa yanafaa kufanywa kubaini iwapo kinga iliotolewa inaweza kuwalinda watu dhidi ya maambukizi ya HIV. 

Takriban watu milioni 37 duniani wanaishi na virusi vya Ukimwi na kuna takriban visa vipya milioni 1.8 kila mwaka. 

Lakini licha ya kupiga hatua dhidi ya Ukimwi, tiba yake na chanjo haijapatikana. 

Dawa kwa jina Prep ni nzuri katika kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo lakini ikilinganishwa na chanjo inafaa kutumiwa mara kwa mara, hata kila siku ili kuzuia virusi hivyo kuzaana . 

Uvumbuzi wa chanjo yake umekuwa changamoto kubwa kwa wanasayansi , kwa sababu kuna aina nyingi za virusi vyake vinavyopatikana katika maeneo kadhaa ya dunia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad