Video: Steve Nyerere Amjibu Muna Aongea Mambo Mazito "Mwanamke Mwenye Busara Lazima Uwe na Khaba"

Video: Steve Nyerere Amjibu Muna Aongea Mambo Mazito "Mwanamke Mwenye Busara Lazima Uwe na Khaba"
Kufuatia mkutano alioufanya muigizaji Muna Love na waandishi wa habari hapo jana na katika maelezo yake akaanika sauti ya muigizaji mwenziye Steve Nyerere ambayo alimpigia simu muda mfupi baada ya mwanae kufariki dunia huko Kenya na kuzungumza nae baadhi ya mambo kuhusiana na kifo hicho cha mwanae.

Katika mazungumzo yake Muna, amekanusha baadhi ya taarifa ambazo zilitolewa na Steve Nyerere zikidai kuwa muigizaji huyo amekubali kushirikiana na Mumewe Peter Komu katika kumzika mtoto Patrick ambaye Muna amekanusha kuwa sio wa Peter bali ni wa Casto Dickson.

Sasa baada ya ubuyu huo kutua mezani kwa Steve Nyerere naye ameamua kuitisha mkutano na waandishi wa habari kupangua hoja zote zilizotolewa na Muna ambazo zinamuhusu yeye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad