VIDEO:Mwanamuziki Tajiri P. Diddy Ampa Wizkid wa Afrika Dili Nono la Mamilioni

Rapa P. Diddy ni moja ya mastaa wakubwa duniani ambao kwa namna moja au nyingine wanasapoti sana muziki wa Afrika na awamu hii ameamua kufanya kazi kwa vitendo zaidi na Wizkid kutoka Nigeria.

P. Diddy kupitia bidhaa yake ya vinywaji vikali vya Cîroc amemtangaza Wizkid kuwa Balozi wa bidhaa hizo ambapo StarBoy mwenyewe amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Kwa upande mwingine pia, Rapa Cassper Nyovest ambaye yeye ni balozi wa muda mrefu amemkaribisha Wizkid kwenye familia hiyo mpya ya Ciroc kwa kumwambia “Y’all already heard da bog!! Cirocboyz worldwide!!! Welcome to the family Wizzy Lion!!! Don’t do drugs!!! Do Ciroc!!! #CirocPhone .@wizkidayo“.

Dili hilo bado halijawekwa wazi lakini vyombo vya habari vinaeleza kuwa na thamani ya dola milioni $1.5 ambayo ni sawa na tsh bilioni 3.3 .

P. Diddy ana-share hisa na kampuni ya Diageo ambayo ndiyo inayozalisha kinywaji cha Ciroc, yeye yupo kwenye upande wa Marketing and Promotion ambako anahusika na masuala yote ya ishu za ubalozi na matangazo ya kinywaji hicho. Tazama video ya Wizkid akitangaza dili hilo



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad