Vita ya Rais Durtete na Wakatoliki yapamba moto Ufilipino

Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte kutamka kwa kinywa chake kuwa Mwenyezi Mungu ni ‘Mpumbavu’ sasa ameibuka na jipya lingine la kujiuzulu urais endapo wakristo nchini mwake watamuonesha picha ya selfie waliyopiga wakiwa na Mungu.

Rais Duterte ambaye amekuzwa na kanisa Katoliki amesema kuwa hakuna Mungu na hata kama angekuwepo hana msaada wowote kwa Wakristo kwani kila siku makanisa yamekuwa yakiongozwa na sadaka zao hivyo haoni kama Mungu wanayemuomba ana msaada wowote.

Akishikilia kauli ya kujiuzulu, Duterte amesema kuwa yupo tayari kujiuzulu urais muda wowote endapo atatumiwa picha ya ‘selfie’ya  Mkristo yoyote yule nchini mwake akiwa amepiga na Mungu ili kuthibitisha uwepo wake.

“Nahitaji shahidi mmoja atakaye niambia ‘Meya’ hawa wapuuzi wanaosali makanisani wameniagiza niende mbinguni nikaonane na Mungu, na hii picha nimekuletea kuthibitisha kuwa Mungu yupo na nimepiga naye selfie hii hapa nimekuletea. bila shaka nitajiuzulu nafasi yangu ya urais.“amesema Durtete alhamisi ya wiki hii kwenye mkutano wa masuala ya mawasiliano na Teknolojia mjini Davao, Ufilipino.

Mwishoni mwa mwezi Juni Rais Duterte alinukuliwa kwenye mkutano huo wa wiki tatu akimtukana Mungu wa Wakristo kuwa ni ‘Mpumbavu’ kwa kile alichokiita kuwa hakutumia akili kumuumba Adam na Eva halafu kuwaweka sehemu moja kama Biblia ilivyoandika.

Duterte amekuwa akilisakama kanisa Katoliki nchini humo kwa kile anachoeleza kuwa haamini Mungu wanayemuamini kama ni Mungu wa kweli ambaye yeye anamuamini.

“Sina imani kama Mungu wao ana msaada wowote, kwani kama kanisa lao lina lengo la kusaidia watu kwanini wanawachangisha pesa kuliendesha?,“amekaririwa Duterte na gazeti la RT.

Rais Duterte ana miaka miwili tu tangu aingie madarakani mwaka 2016 lakini amekuwa mwiba kwa kanisa katoliki ambalo ndio dhehebu lenye waumini wengi nchini Ufilipino ambao wanakadiriwa kuwa milioni 80 kati ya watu milioni 104 ni wakatoliki.

Vita ya Duterte na kanisa katoliki ilianzia mwaka 2016 mapema baada ya kuanza kampeni ya kupiga risasi watu wote wanaojihusisha na madawa ya kulevya ambapo Kanisa Katoliki lilimpinga na kumuita muuaji kwani watu hao walitakiwa wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria kama katiba ya nchi hiyo inavyotaka.

Hata hivyo Duterte awali alishawahi nukuliwa akisema kuwa Mungu wa Wakatoliki sio Mungu wa kweli ndio maana wanaruhusu maovu na kuponda baadhi ya maandiko matakatifu kutoka katika Biblia.

Hadi sasa Duterte ameibua mjadala mkubwa nchini Ufilipino na amekataa katu katu kuwaomba radhi wakristo nchini humo na tayari wataalamu wa masuala ya kisiasa wameleeza kuwa rais huyo ana nafasi ndogo sana kushinda uchaguzi  mkubwa ujao.

Duterte alishawahi kutoa matamshi makali kwa Rais Obama mwaka 2016 kwa kumuita kuwa ni mtoto wa kahaba na hana muda wa kukutana naye ingawaje mwaka huo huo walikutana na Obama.

Trump ameshamuonya tayari Duterte kwa kitendo cha kuua watu kiholela lakini hajamjibu mpaka leo. Ufilipino linatajwa kuwa taifa linaloongozwa kidikteta ingawaje rais Duterte amekuwa akiwabeza wanaomuita yeye ni Dikteta.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad