Wakulima Waonywa Kuchanganya Nafaka na Mchanga

WADAU wanaojishughulisha na ununuzi wa mazao mbalimbali mkoani  hapa  wamewataka wakulima kuacha tabia ya kuchanganya nafaka na mchanga kwa kuwa  hali hiyo imekuwa ikiondoa ubora  na thamani wa mazao.

Ushauri huo ulitolewa na Meneja wa kiwanda cha The Agro Processing Africa Purimui Suvuiiyu  baada ya kubainika baadhi ya wakulima wa zao la choroko kuwa na tabia ya kuchanganya  nafaka na mchanga kwenye magunia kwa lengo la kuongeza  uzito.

Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wanunuzi wakuu wa nafaka kutoka kampuni ya Export Trading LTD yenye makao makuu ya jijini Dar- es- salaam, meneja huyo alisema kuwa baadhi ya wakulima wamekuwa wakiongeza uzito kwa kuchanganya kwenye nafaka hizo kwa kuweka mchanga.

Alisema hali imekuwa ikishusha thamani ya zao hilo.

“Kiwanda chetu kinajishughulisha na shughuli za uchakataji wa choroko ambazo tunanunua kutoka kwa wakulima, kinachosikitisha baadhi yao siyo waaminifu wamekuwa wakichanganya mchanga na nafaka zingine ambazo siyo za choroko na kusababisha kiwanda kuingia kwenye hasara kubwa,”alisema.

Alisema kuwa kiwanda hicho kinauza choroko zake hadi nchi za nje hivyo kitendo cha wakulima kuchanganya zao hilo na vitu vingine vinaweza kushusha thamani  kwenye masoko ya  nje ambao wamekuwa wakinunua.

Naye, Meneja  Uhusiano wa Kampuni ya Export Trading Group, Fatuma Ally alisema choroko inayonunuliwa toka kwa wakulima wadogo wakati mwingine inakuwa haina ubora wa kutosha na kutokidhi vigezo kwenye masoko ya nchi za nje.

Alisema hukutwa choroko zimechanganywa na mchanga hivyo kusababisha ufanyaji wa kazi kubwa wa usafishaji kabla ya uchakataji na pia kupunguza kiwango cha choroko iliyonunuliwa.

Hata hivyo alisema kwa upande wao wa kampuni ya Export imekuwa ikinunua mazao mbalimbali kwa ajili ya kuwakomboa wakulima katika kujipatia kipato cha bei pamoja na soko.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad