Waliohama Upinzani Walamba Shavu Kwa JPM


NA FATUMA MUNA
Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya wakuu wa Mikoa, wa Wilaya na Makatibu tawala nchini ambapo amewateua wanasiasa watatu waliowahi kuwa vyama vya upinzani kabla ya kuhamia CCM kwa nyakati tofauti tofauti.


Akitangaza mabadiliko hayo leo Julai 28, Rais Magufuli ametangaza kumteua David Kafulila kuwa Katibu Tawala, Mkoa wa Songwe ambapo kabla ya kuhamia CCM Kafulila aliwahi kuwa mbunge wa NCCR-Mageuzi jimbo la  Kigoma Kusini.

Kafulila aliyepata umaarufu baada ya kuibua sakata ufisadi wa Escrow, alitangaza kujiengua CHADEMA, Novemba 22, 2017, akidai vyama vya upinzani havina dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi na kwamba muda ukifika atatangaza anakokwenda.

Hata hivyo Novemba 24, 2017, Kafulila aliibukia kwenye mkutano wa kampeni wa CCM Kata ya Mbweni na kutangaza kujiunga na CCM alipoitwa jukwaani na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

Pia Rais amemteua Moses Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Machali aliwahi kuwa mbunge wa Kasulu Mjini kupitia (NCCR-Mageuzi) kabla ya kuhamia ACT-Wazalendo na baadaye CCM.

Rais Magufuli pia amemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA kabla ya kuhamia CCM Nov 21, 2017, Patrobas Katambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad