Wanajeshi wanne wa Ugana Wafariki Kwenye Mapigano Kati ya Vikosi vya Uganda na DRC Katika Ziwa Edward

Wanajeshi wanne wa Ugana Wafariki Kwenye Mapigano Kati ya Vikosi vya Uganda na DRC Katika Ziwa Edward
Watu 7 wamefariki wakiwemo wanajeshi 4 wa Uganda katika mapigano kwenye ziwa Edward kati ya vikosi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Uganda, kwa mujibu wa afisa wa Congo aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP.

Ziwa Edward lipo katika mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Kiongozi kutoka Beni, Donat Kibwana, amenukuliwa na AFP akisema kuwa mashua ya kupiga doria ya Congo ilishambuliwa Alhamisi asubuhi na boti la kupiga 'doria la Uganda'.

Boti la Uganda lilizama na wanajeshi wanne wa taifa hilo na raia watatu walifariki, aliongeza.

Twaweza: Watanzania 'hawako tayari kuandamana'

Onyo la Macron kuhusu vituo vya wahamiaji Afrika

Jaribu Muliwavyo, mbunge kutoka eneo hilo, amekiambia kituo kimoja cha redio Congo kwamba mapigano hayo yanatokana na mzozo wa haki za kuvua.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad