"Wanampotosha Rais" - Silinde


Mbunge wa Mbozi  Magharibi, David Ernest Silinde amebainisha kuwa wasaidizi wengi wa Rais Magufuli  wamekuwa wakimpotosha kiongozi huyo kwa kutomwambia ukweli sehemu zenye mapungufu ili tu kumfurahisha.


Kulia ni Rais Magufuli, kushoto ni Mbunge wa Mbozi Magharibi David Ernest Silinde.

Akizungumza na www.eatv.tv amesema viongozi hao wamekuwa wakidhani kwamba kuwadhibiditi Upinzani watakuwa wanamfurahisha Rais na badala yake wanampotosha kwa kutosema ukweli.

Silinde amesema kwamba kuna maeneo ambayo Rais hashauriwi vizuri lakini kwa kuwa viongozi wake wanahisi kwamba kuzuia hotuba za upinzani ni suluhisho ndiyo maana kuna mambo yanaanzisha na yanagota kabla ya kufika mwisho.

Pamoja na hayo kiongozi huyo amesema ipo haja ya kuwa na mapendekezo ya mabadiliko ya kikanuni kusiwepo na mamlaka ambayo itaweza kuzuia  hotuba za kambi ya upinzani, kamati au hata zile za kiserikali kwani utaratibu wa sasa unatokana na kanuni hizo.

EATV
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad