Kampuni ya Johnsons & Johnsons imeamriwa kulipa fidia ya dola za Kimarekani bilioni 4.7 kama fidia na faini kwa wanawake 22 waliodai kuwa bidhaa za talc za kampuni hiyo zimewasababishia saratani ya ovari.
Baraza la Mahakama Missouri huko Marekani limeamuru walipwe dola za kimarekani milioni 550 kama fidia na wakaongeza dola bilioni 4.1 kama adhabu ya fidia.
Uamuzi huo unakuja wakati ambapo kampuni hiyo kubwa ya dawa ikipambana na kesi 9,000 zinazohusisha bidhaa yake maarufu ya poda.
Katika kesi hiyo iliyodumu wiki sita, wanawake hao na familia zao wamesema kuwa wamepata saratani ya ovari baada ya kutumia poda ya Johnsons na baadhi ya bidhaa zake za talc kwa miongo kadhaa.
Mawakili wa familia hizo wanasema kuwa kampuni ya Johnsons ilikuwa inatambua kuwa bidhaa yao ya poda ya talc ilikuwa na madini mabaya ya 'asbestos' tangu mwaka 1970 lakini ilikosa kuwaonya watumiaji kuhusu athari.
Kampuni hiyo ilikana kuwa bidhaa zake zimewahi kuwa na madini mabaya ya asbestos na walisisitiza kwamba bidhaa hizo hazileti saratani.
Kampuni hiyo kubwa ya dawa iliongeza kwamba tafiti mbali mbali zimeonyesha kuwa poda yao ni salama na wakasisitiza zaidi kuwa uamuzi huo ni matokeo ya uamuzi usiotenda haki.
Malipo hayo ndiyo ya juu zaidi kwa J&J kuwahi kuamriwa kulipa kama fidia kutokana na bidhaa zake na tuhuma kwamba huwa zinasababisha kansa.
Katika kesi iliyopita mwaka 2017 jopo la mahakama Calfonia liliiamuru kampuni hiyo kulipa tozo ya dola za kimarekani 417 kwa mwanamke ambaye alisema amepata saratani ya mayai ya uzazi baadha ya kutumia bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo poda yake ya watoto (Johnsons baby powdwer)
Hata hivyo baadaye hakimu alibadiliuamuzi huo japo bado kampuni hiyo ina kesi kadhaa ambazo bado hazijatolewa uamuzi.
Adhabu za kulipa fidia mara nyingi huwa zinapunguzwa kwa hakimunwa kesi hiyo au kukata rufaa, na J&J imefanikiwa kubadili maamuzi ya kesi kadhaa huku baadhi ya hukumu hizo wakitoa vigezo vya matatizo ya kiufundi.