“Wasanii Tupunguze Kiki Tufanye Kazi Zaidi”- Irene Paul


Muigizaji wa Bongo movie Irene Paul ameibuka na kuwashauri wasanii wenzake kuachana na kiki na kuanza kufanya kazi zao za sanaa kwa nguvu zaidi.

Wasanii wengi wamekuwa na mtindo wa kutengeneza skendo fulani (kiki) ziwe za kimapenzi au bifu lakini skendo zitakaziweza kuwaletea attention fulani kutoka Kwa vyombo vya habari au mitandao ya kijamii ili watakapotoa kazi zao zifanye vizuri.

Irene Paul amewataka wasanii wenzake kuacha kuzidisha sana kiki kama njia ya kutafuta attention kwani inakuwa inaharibu kazi zao kwani jitihada hivyo ya kiki wangeielekeza katika kutengeneza kazi Debye unitary basi mambo yangekuwa mazuri;

Nafikiri tumesha hustle sana Kwenye hii gemu kwa njia tofauti na umri haurudi nyuma bali unasogea so I think it’s about time tufanye kazi zaidi kwani ndio kitu pekee kilichobaki.

Waliojiuza wamejiuza sana na waliokaa uchi wamekaa uchi sana na waliotengeneza skendo wametengeneza skendo za kutosha lakini wamepata nini out of it?.

Lakini pia Irene Paul amewataka Bongo movie wenzake waelekeze nguvu zao Kwenye kufanya kazi zaidi ili kuitudisha Bongo movie Kwenye ramani:

Umefika wakati tufanye kazi Bongo Movie Industry sio ya kipindi kile wakati inaanza kuna mapinduzi makubwa twende na wakati Tanzania tuna vipaji lakini tuna lack Knowledge na ubunifu kwaiyo cha muhimu kufanya kazi kwa bifu bidii ili kufika malengo”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad