Msanii wa bongo Fleva Shilole amefunguka kuwa ameamua kuwekeza nguvu zake nyingi kwenye ujasiriamali kwa kuwa anajua kuna leo na kesho mziki unaweza ukabuma kwahiyo biashara zake zitakuwa msaada kwake kwa kuendeleza maisha.
Akizungumza na www.eatv.tv amesema muziki unalipa sana na unalevya kwakua wasanii wengi wanajua muziki utakuwa biashara yake ya milele na kusahau kuna kubuma kwa mziki kwahiyo mwisho wa siku muziki unabuma uku hujawekeza ndo kinakuwa chanzo cha msanii kuishi maisha mabovu.
Shilole amesema mtu anapokuwa marufu lazima aishi maisha ambayo yapo juu kwa gharama kwahiyo kwa siku unakuta mtu anatumia pesa nyingi kuliko anayoingiza kwahiyo kama muziki ukibuma na maisha yapo juu lazima uyumbe.
“Wasanii wasilewe na pesa za 'show' tu inatakiwa kufanya biashara tofauti tofauti ili hata kama muziki utakubumia iwe rahisi kuishi maisha mazuri maana kuna wasanii zamani walikuwa wanafanya vizuri na walikuwa na pesa kwakua tu walijisahau na hawakuogopa kesho yao muziki ulipobadilika tu wakaanza kuishi maisha ya kawaida,”amesema shilole.
Ameongeza kwa kusema vijana wengi wa kileo wanapenda maisha mazuri lakini wanachagua kazi, inatakiwa vijana kama taifa la leo wasichague kazi, kazi ni kazi kikubwa iwe halali ,watu waliofanikiwa wengi walianzia sehemu za kawaida baadaye ndio wanakuja kupata sehemu nzuri kwahiyo vijana waache kuchagua kazi.