Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa watanzania wengi wana tabia ya kukatishana tamaa, pindi wanapoona mtu akifanya jitihada za kujikwamua kimaendeleo.
Rais Magufuli ametoa wito huo leo, wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Reginald Mengi kinachoelezea historia ya maisha yake kinachoitwa ‘I can, I must, I will’ ambacho amekiandika mwenyewe.
Rais Magufuli amesema kuwa imejengeka tabia ya watanzania kukatishana tamaa katika jitihada za kujikwamua kiuchumi, na kusababisha wasio jiamini kuishia njiani katika mapambano dhidi ya umaskini.
“Watanzania tuache tabia ya kukatishana tamaa, na nina fahamu katika kukatisha tamaa wapo wengi walioambiwa hawawezi kufanya kazi ya madini lakini yote hayo ni kwasababu ya watu kutaka kukatisha tama”, amesema Rais Magufuli.
Kitabu cha Dkt. Reginald Abraham Mengi kimezinduliwa rasmi leo na Rais Dkt. Magufuli akipatiwa nakala ya kitabu cha 'I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success' pamoja na viongozi wengine wakuu waliohudhuria.