DAR: Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Kamishna wa Uhamiaji kutotoa kibali kwa Mtanzania yeyote kuondoka nchini kwa madai ya kupata kazi nje ya nchi bila kujiridhisha kuwa anayo mikataba ya sehemu anayokwenda kufanya kazi
Amemtaka pia Kamishna wa Uhamiajia ajiridhishe kwa kufanya mawasiliano na Balozi husika katika nchi ambayo mtanzania huyo atadai anaenda kufanya kazi
Kauli hiyo ameitoa wakati wa shughuli ya maadhimisho ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu nchini jana Julai 30 katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Pia amesisitiza kuwa Serikali haikatazi Watanzania kwenda kufanya kazi nje ya nchi bali kinachotakiwa ni kufuata utaratibu kutokana na nchi kuendelea kuathirika na watu kusafirishwa kiharamu na kwenda kuteswa
Aidha, Waziri Lugola ameagiza msako wa nyumba kwa nyumba, mashamba kwa mashamba, viwanda kwa viwanda na sehemu zote zinazotoa ajira kuangalia kama kuna Wahamiaji haramu walioajiriwa
Katika hatua nyingine kwenye maadhimisho hayo, Waziri Lugola amemfuta kazi Mjumbe wa Sekretarieti ya kupinga usafirishaji Haramu wa binadamu kwa kushindwa kujua idadi ya vyombo vinavyotakiwa kutaifishwa - #regrann