Watu Wanne Wanusurika Kuchomwa Moto Kisa Ushirikina

Watu wanne wanusurika kuchomwa moto kisa ushirikina
Watu wanne wamenusurika kuchomwa moto kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ushirikina katika hifadhi ya msitu wa Isawima kijiji cha Mpanda Mlowoka wilayani Kaliua mkoani humo.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kamanda wa polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi EMMANUEL NLEY amesema tukio la mauaji lilitokea usiku wa July 14 ambapo marehemu alivamiwa na kuuawa kwa kukatwa shingo na kitu chenye ncha kali.

Kamanda NLEY anaendelea kuelezea tukio lingine la wakina mama wanne walionusurika kuchomwa moto

Katika tuki hilo jeshi la polisi limefanikiwa kukamata pikipiki mbili moja ikiwa ni mali ya Mtemi wa sungusungu wa eneo hilo pia kuwatia nguvuni watu kumi na sita.

Mbali na matuki hayo pia mnamo july 14 huko katika kata ya ipuli mjini Tabora mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la REGINA ATHUMANI aliuawa kwa kupigwa kisha kunyongwa na mumewe

Jeshi la pilisi mkoani Tabora limewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheia mkononi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad