Raia wa Uganda wanaotumia mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp na Twitter kuanzia leo watalazimika kulipa kodi ili kutumia mitandao hiyo.
Serikali ya Uganda inatarajia kukusanya kodi ya mamilioni ya dola kwa mwaka kupitia kodi hiyo mpya.
Wakosoaji wanaiangalia kodi ya kutumia mitandao ya kijamii kuwa ni njama ya Rais Yoweri Museveni ya kufanya maisha ya wapinzani wake kuwa magumu.
Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, anaishutumu mitandao ya kijamii kwa kusambaza taarifa za uongo na uvumi.
Kila mtumiaji wa mitandao hiyo nchini humo, atalipa shilingi 200 kwa siku na kampuni ya simu zimetwikwa jukumu la kukusanya kodi hiyo.
Inakadiriwa watu milioni 17 kati ya Waganda milioni 40 wanaotumia Intaneti kupitia simu zao za mikononi.
Watumiaji wa Facebook, WhatsApp na Twitter Waanza Kulipa Kodi Uganda
July 02, 2018
Tags