Wawindaji Wawili wa Faru Waliwa na Simba

Wawindaji Wawili wa Faru Waliwa na Simba
Takribani majangili wawili wa vifaru wame raruliwa na kuliwa na simba katika mbuga ya wanyama huko Afrika ya kusini, maafisa wamesema.

Askari wa doria waligundua mabaki ya watu wawili, na wengine wanahisi ni mabaki ya watu wa tatu, katika mbuga ya wanyama ya Sibuya karibu na Kusini-Mashariki mji mwa mji wa Kenton

Bunduki yenye nguvu kubwa na shoka pia vili kutwa hapo.

Kwa nini huenda ndizi zikatoweka duniani

Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi afariki kwa kupigwa risasi

Katika miaka ya hivi karibuni, Ujangili umeongezeka sana Afrika ya Kusini, ili kutokana na kuongezeka kwa hitaji la pembe za vifaru huko bara la Asia.

Kwa upande wa China, Vietnum na sehemu nyingine nyingi pembe za vifaru zinaaminika kuwa na sifa ya kuongeza hisia za mapenzi.

Mmiliki wa Hifadhi wa Sibuya, Nick Fox katika taarifa yake kwenye ukurasa wa Facebook wa mbuga hiyo amesema watu hao wanao sadikiwa kuwa ni majangiri waliingia katika mbuga hiyo jumapili usiku au mapema siku ya Jumatatu asubuhi.

"Walikosea na kuingia kwenye eneo la kujidai la simba, ni eneo kubwa hivyo hawakuwa na muda mwingi, " Bwana Fox aliliambia Shirika la habari la AFP.

"Hatuna hakika ni watu wangapi walikuwa - kwani kuna mabaki kidogo sana ya miili yao. "
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad