Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vyama vya ushirika duniani yaliyofanyika jijini Mwanza Majaliwa amesema, viongozi ambao wanasafilisha fedha za vyama vya ushirika kinyume na utaratibu na baadae kusema kuwa wamevamiwa na kuporwa fedha hizo watawajibishwa kisheria.
"Wizi na ubadhirifu ulioshamiri unadhoofisha maendeleo ya ushirika mjitathimini na kusababisha hasara kubwa na kuwa mzigo wa serikali ili kulipa fedha hizo", amesema Waziri Mkuu Majaliwa
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa serikali itaangalia upya mpangilio wa mnada wa kahawa mkoani Kilimanjaro na badala yake ufanyike katika mikoa husika inayozalisha kahawa ili mkulima afike ,mwenyewe kwenye mnada na kushuhudia bei halisi.