Maafisa wa kupambana na ufisadi nchini Malaysia wamemkamata Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia kwa madai ya ufisadi na kumfikisha mahakamani ambapo alikanusha madai hayo.
Razak anadaiwa kufuja pesa kutoka kwenye hazina ya serikali alipokuwa madarakani na iwapo atapatikana na hatia basi huenda akapata kifungo cha miaka 20 jela.
Kesi kwa Razak zilianza punde tu aliposhindwa uchaguzi mwezi May, ambapo alizuiliwa kuondoka nchini humo huku shirika la kupambana na rushwa likianza kumhoji na kupekua nyumba zake kama sehemu ya uchunguzi.
Razak aliachiliwa huru wa muda baada ya kulipa dhamana ya $250,000
Waziri Mkuu wa Zamani wa Malaysia Apandishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Ufisadi
July 04, 2018
Tags