Waziri Ummy Mwalimu Awasimamisha Kazi Walioshiriki Kusafirisha Shehena Ya Mirungi kwa Kutumia Gari ya Kubebea Wagonjwa

Waziri Ummy Mwalimu Awasimamisha Kazi Walioshiriki Kusafirisha Shehena Ya Mirungi kwa Kutumia Gari ya Kubebea Wagonjwa
Ikiwa zimepita siku mbili tangu kuripotiwa kwa tukio la kukamatwa kwa gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ likiwa limebeba shehena ya mirungi, Wilayani Tarime mkoani Mara, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza kusimamishwa kazi wote waliohusika.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo akiwa ziarani wilayani Itilima mkoani Simiyu katika uzinduzi wa tuwatumie wahudumu wa Afya ngazi za jamii, ambapo amesema kuwa hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mtumishi yeyote wa sekta ya afya atakayekwenda kinyume na utaratibu wa utoaji huduma.

“Ni marufuku gari la kubeba wagonjwa kubeba mkaa wala bidhaa nyingine, nalipongeza jeshi la polisi mkoani Mara kwa kuchukua hatua na mkurugenzi wa mkoa wa Mara nakuagiza kuchukua hatua mara moja usisubiri kusikiliza popote”, amesema ummy.

Julai 10, 2018 Askari polisi mkoani Mara walilikamata gari la kubeba wagonjwa mkoani humo lililokuwa limesheheni shehena la mirungi, ambapo dereva amewekwa mahabusu akisubiri kufikishwa mahakamani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad