Waziri wa Afya Aionya TFDA "TFDA Isiwe Kikwazo Katika Juhudi za Rais Magufuli”

Waziri wa Afya Aionya TFDA "TFDA Isiwe Kikwazo Katika Juhudi za Rais Magufuli”
Waziri wa Afya, Maendelao ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekabithi vyeti vya ithibati kwa kiwango vha kimataifa ambapo ameitaka Mamlaka hiyo kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji nchini hususan viwanda vya kuzalisha dawa.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kukabidhi vyeti vya ithibati kwa kiwango cha kimataifa ISO 17025 kwa maabara ya chakula na maikrobailojia za TFDA.

“TFDA isiwe kikwazo kwa wawekezaji nchini hususan viwanda vya kuzalisha dawa ili kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ya kuelekea uchumi wa viwanda.” amesema Waziri Ummy

“TFDA mnawajibu wa kuwawezesha wafanyabiashara kutoa bidhaa zao wanazozileta nchini mapema zaidi mara wanapokuwa wamejiridhisha na ubora unaokidhi afya za watanzania na kuwapa vibali mapema”, amesema Ummy.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad