Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Milioni 2 za Idris Sultan

Malkia wa filamnu Bongo Wema Sepetu amefunguka kuhusu fedha za Idris Sultan alizodai kuwa atamlipia kama faini ya kwenye kesi yake aliyokutwa na hatia ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Akiongea na SNS TV kwenye sherehe ya 40 ya mtoto wa Zamaradi Mketema, Madam Sepenga amesema kuwa yale yalikuwa ni maneno tu kutoka kwa mchekeshaji huyo ambaye waliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

"Maneno tu, Idris munamjua. Maneno tu (akacheka kidogo)." Wema akaendelea kwa kusema, "Maneno tu hivyo."

Ijumaa iliyopita ya Julai 20 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  ilimpiga faini Wema ya shilingi milioni mbili au kifungo cha mwaka mmoja jela, hapo ndipo aliibuka Idris na kudai kuwa atamlipia faini hiyo mrembo huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad