Mwenyekiti wa Kamati Maalum kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abbas Tarimba, amesema kuwa tayari wameshakamilisha kulipa fedha zote ambazo zilikuwa ni malimbikizo ya madeni kwa wachezaji wao, imeelezwa.
Tarimba ambaye aliteuliwa na uongozi wa Yanga kupitia Mkutano Mkuu wa klabu uliofanyika Juni 10 2018 jijini Dar es Salaam, imeelezwa kuwa kwa kushirikiana na aviongozi walio kwenye kamati hiyo wamekamilisha madeni hayo.
Klabu ya Yanga imekuwa inapitia kipindi kigumu hivi sasa ikihaha kuwaongezea mikataba wachezaji wake ambao wengi wamemaliza mikataba lakini sasa kamati hiyo chini ya Tarimba imeanza kuonesha kupambana.
Baada ya kukamilisha madeni hayo, Tarimba ameeleza kuwa hivi sasa wanazidi kujipanga katika kuweka nguvu zao zote katika usajili wa wachezaji ili kukiboresha kikosi chao ambacho kinakabiliwa na mashindano ya kimataifa.
Ikumbukwe Yanga walio kambi hivi sasa hapa wanajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya iliyopo nchini hivi sasa kwa ajili ya michuano ya KAGAME.