Yanga Yaweka Wazi Kuhusu Obrey Chirwa

Yanga Yaweka Wazi  Kuhusu Obrey Chirwa
Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka jambo kuhusiana na aliyekuwa mchezaji wake, Mzambia, Obrey Chirwa ambaye hivi sasa amejiunga na Ismailia ya Misri.

Kwa mujibu wa Hussein Nyika kupitia kipindi cha michezo, Radio One, amesema Chirwa alimaliza mkataba na Yanga hivyo wasingeweza kumzuia asifanya mazungumzo na timu zingine.

Nyika amefunguka kwa kusema yeye kama kiongozi wa Yanga na klabu kwa ujumla wanamtakia kila lililo jema huko alipo katika kazi yake ya mpira baada ya kufikia mwafaka na timu yake mpya ya Ismailia kuichezea.

Mbali na kuondoka kwa Chirwa Yanga, Nyika amesema mchezaji huyo alikuwa ni moja ya waliokuwa bora kwenye kikosi cha timu yao kutokana na mchango pamoja na umahiri wake ndani ya Uwanja.

Chirwa ameondoka Yanga akiwa amechangia kuipatia ubingwa wa Ligi Kuu Bara katika msimu wa 2016/17 mbele ya watani zao wa jadi Simba ambao waliambulia nafasi ya pili.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad