Akiongea mbele ya umma Zamaradi anasema kuwa mume wake ni kama baba kwake kutokana na ukweli kuwa amekuwa mtu muhimu , anaemuelewa na kumjali kwa kila kitu tangu amekuwa nae katika maisha yake.
Zamaradi pia amesema kuwa siri kubwa ambayo wengi inawezekana walikuwa hawaijui ni kwamba , mume wake ndie alikuwa akimkanda na maji ya moto kwa kipindi chote alichojifungua mtoto wake huyo wa kiume.
Zamaradi pia amesema kuwa kwake sio shida kuzaa na kuendelea kuongeza familia na mwanaume huyo hata kama anawatoto watatu tayari.
Amenikubali kama nilivyo na kunipenda na mimi nimemkubali kama alivyo na kumpenda pia,mpaka hapa tulipo tuna familia pamoja na tunategemea kuongeza familia pamoja ,nataka tu kumwambia kuwa nina kupenda sana na asante kwa kila kitu.
kitu ambacho wengi hamjui ni kwamba kipindi chote cha kujifungua nimekuwa nikikandwa na yeye na hii kutokana na kwamba hakukuwa na mzazi wa kunikanda mimi, wazazi wangu wote walishatangulia mbele ya haki