Mwanadada mpambamaji hapa nchini Zamaradi Mketema ni miongoni mwa Watanzania Walioguswa na hali aliyonayo mtoto wa Muna Love na kuamua kuhamasisha watu kupitia mitandao ya kijamii kuchangia fedha za matibabu ili kusaidia kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Mtoto wa Muna yupo ICU katika hospitali ya nairobi kwa siku ya sita sasa na kupitia matibabu anayopatiwa hadi sasa gharama imefikia milioni 22 .
Kupitia ukrasa wake wa instagram Zamaradi ameandika hivi;
"Nimezaa naelewa unachopitia,
Wapenzi mwenzetu yuko kwenye mtihani mzito, anauguza mtoto wake na yuko Hospitali Nairobi huku mtoto akiwa ICU almost siku ya sita leo, tunaelewa kuuguza ni nini, hata kama una kitu bado hakitatosha, Dawa anayotumia mtoto kwa siku hizi sita mpaka sasa Bill ni milioni 22!karibu na bado inaongezeka, nimeongea nae kuhusu kusaidia pale tunapoweza na kakubali, na nimeomba ACCOUNT YAKE YA BENKI ambayo hela itamfikia moja kwa moja, hivyo kwa yeyote atakaeguswa kuna NAMBA ambazo asubuhi utazioata kupitia page yangu na ya @munalove100 ambayo ni ACCOUNT YA BANK ya mtoto mwenyewe na unaweza kutuma kiasi chochote moja kwa moja itamfikia.
Naomba nifungue dimba hili kwa kuchangia Milioni moja, na nimeongea na WEMA pia nae kachangia ya kwake ambazo tunatuma moja kwa moja kwenye account siku ya kesho, tunaomba na wewe utakaeguswa tafadhali usaidie kwa kiwango chochote utakachoweza, ndio maana ya kushirikiana kwenye matatizo. Kumbuka kabla ya hapa alimuuguza mwanae kwa muda mrefu sana hivyo ifike mahala tusaidie kuubeba huu mzigo, na namba ya account ni yake yeye hivyo itamfikia moja kwa moja.
#kutoanimoyosiutajiri"
Zamaradi Ahamasisha Kuchangia Matibabu ya Mtoto wa Muna Love... Achangia Milioni 1 Wema Naye Atoa Mchango Wake
July 03, 2018
Tags