Zitto Kabwe Amtupia Dongo Mwigulu Baada ya Kutumbuliwa...Pole Pole Amvaa Zitto na Kumjibu


BADA ya Rais Magufuli kutangaza mabadiliko madogo katika Wizara kadhaa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuachwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe wameanza kuvutana mitandaoni kuhusu kuachwa kwa Mwigulu.

Kupitia mtandao wa wa Twitter Zitto Kabwe amemkaribisha, Dkt. Nchemba kwa kumwambia sasa ni wakati wake wa kuwatumikia wananchi na kwamba msimamo wake ndiyo uliomponza.

Kufuatia kauli hiyo, Humphrey Polepole katika ukurasa wake, ameamua kumvaa Kiongozi huyo wa ACT kwa kumuita mzee wa kurukia treni kwa mbele 

Rais amefanya mabadiliko kutokana na dhamana aliyopewa na Katiba na si vinginevyo na kumtaka asipotoshe watu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad