Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amepingana na maamuzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuwapiga chini wachezaji 6 Simba katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Rage amesema maamuzi hayo ni ya kuwakosea wachezaji na badala yake akishauri ni vema wangepewa onyo.
Kiongozi huyo wa zamani Simba ameeleza kitendo cha Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike kuwapa adhabu kali wakati wakiwa hawana rekodi ya kufanya hivyo si cha busara na badala yake alitakiwa aende nao taratibu.
Aidha, ameshauri ni vema zaidi kama wangeweza kutwafutwa kupewa onyo na ikiwezekana walau kupigwa hata faini jambo ambalo lingewaamsha na kuwa wanawahi kwa siku za usoni.
"Ni jambo ambalo si sahihi kabisa, nadhani wangeweza kufuatwa na kupewa hata onyo kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kuchelewa. Au kama ingewezekana wangepigwa hata faini" alisema.