Afrika Kusini yakosoa ujumbe wa Trump


Afrika Kusini inamshutumu Rais Donald Trump kwa kuchochea chuki baina ya watu wa rangi mbali mbali katika kujibu ujumbe wake wa tweet uliyokuwa unaelezea kuwa wakulima wazungu walikuwa wana nyang’anywa ardhi na kuuwawa.

Rais Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa tweet Jumanne kwamba amemwagiza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo “kufuatilia kwa karibu sana yanayojiri Afrika Kusini katika unyang’anyaji na utaifishaji wa ardhi na mashamba na vitendo vya mauaji ya kiwango cha juu cha wakulima.

Ujumbe huo wa Tweet uliotolewa na Trump unaelekea kuwa ni majibu dhidi ya pendekezo la Rais Cyril Ramaphosa juu ya sera ya mageuzi ya ardhi nchini Afrika Kusini.

Serikali ya Afrika Kusini imemjibu Trump katika ujumbe kupitia akaunti yao rasmi, ikisema “inapinga kikamilifu uelewa huu finyu ambao unataka kuligawanya taifa letu na kutukumbushia ukoloni.”

“Afrika Kusini itaongeza spidi katika hatua yake ya kuleta mageuzi katika sera ya ardhi kwa uangalifu na kwanjia ya kuwanufaisha watu wote bila ya kuligawanya taifa letu,” ujumbe uliofuatia ulieleza.

Rais Ramaphosa hivi karibuni alitangaza kuwa atapeleka ombi la kurekebisha katiba ili kuwezesha hatua ya ardhi kuchukuliwa na kugawanywa tena bila ya wamiliki wa ardhi hizo kulipwa fidia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad