Aika Afunguka Kuhusu Kuzaa Nje ya Ndoa

Aika Afunguka Kuhusu Kuzaa Nje ya Ndoa
SI wageni machoni kwako, masikioni mwako na pengine unawapenda. Wana ‘hit song’ nyingi, zikiwemo Lini, Kamatia, Feel Good na wimbo wao mpya uitwao Fella, unakimbiza mbaya.  Kwa upande wa albamu wamefanya mbili, ambazo ni AIM (Above Inna Minute) na Hold Me Back, zaidi wanamiliki studio iitwayo The Industry ambayo ndani yake ina Lebo iitwayo Aika Calvin Marealle.

Nakupa zaidi; Kundi hili ni Waafrika wa kwanza kufanya shoo nchini Israel, na rekodi hii waliiweka baada ya kutoa wimbo uitwao Feel Good, mwaka 2016. Wapo kwenye uhusiano kwa takriban miaka kumi na wamebahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Gold aliyezaliwa Desemba, mwaka jana.

Bila shaka ushafahamu ninaowazungumzia, ni Aika Marealle na Emmanuel Mkono wanaounda kundi liitwalo Navy Kenzo. Bila shaka kwa mpenzi wa burudani kuna mengi ungependa kusikia kutoka kwao. Mikito Nusunusu inakusogezea Aika, ana mengi ya kukujuza ambayo pengine huyafahamu kuanzia kwenye kazi zao na ‘life style’ yao, usihamishe ukurasa:

MIKITO: Aika vipi kuhusu mapokezi ya wimbo wenu wa Fella?

AIKA: Kiukweli mapokezi ni mazuri. Wimbo umeenda kiasi cha kufika kwenye ‘platform’ kubwa. Tukizungumzia Uingereza, umesumbua zaidi ya mwezi mzima kwenye chati za muziki za BBC, lakini pia unafanya vizuri Hispania, Russia na Ufaransa. Ni juzi tu tumepewa takwimu kwamba wimbo wetu ni miongoni mwa nyimbo zilizopakuliwa sana kwenye mitandao ya nyimbo Ufaransa.

MIKITO: Mapokezi haya yanawapa picha gani ikiwa mlikaa muda mrefu bila kufanya kazi?

AIKA: Tumegundua kwamba ‘fun base’ yetu inazidi kuongezeka. Watu wanavutiwa na vingi kutoka kwetu. Maisha tunayoishi na mengine mengi. Tumejifunza pia ukiwa na msingi mzuri hata ukikaa miaka miwili ukirudi mashabiki watakupokea tu.

MIKITO: Mnaamini ‘views’ nyingi za YouTube zinatoa picha kwamba wimbo unafanya vizuri?

AIKA: Hapana. Tena kweye hili ninapenda kuwashauri wanamuziki wengine kujiimarisha kwa mashabiki na kuhakikisha kazi zao zinawafikia na pia kwa watu wa ‘media’. Si kila anayetazama wimbo wako YouTube anapenda kazi yako au atapakua muziki wako na kukusapoti.

MIKITO: Kwa sasa Navy Kenzo ni kundi kubwa Afrika, vipi kwa upande wa menejimenti yenu, ipo imara kiasi gani kuhakikisha kwamba mtaendelea kuwa sokoni?

AIKA: Ukiangalia kabla tukiwa wenyewe, yaani Navy Kenzo kama Navy Kenzo chini ya The Industry bado tulikuwa tunafanya vizuri na tumefika mbali. Sasa vipi kwa sasa tulipoungana na Salam Sk na meneja mwingine kutoka Marekani? Hakika ni zaidi ya mwanzo, unaweza kuona picha ya namna tulivyo imara kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad